Rais mstaafu Uhuru Kenyatta anasema alifanya kila awezalo kumuunga mkono marehemu Raila Odinga katika azma ya urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2022. Uhuru amepuuza ukosoaji kwamba alishindwa kufanya vya kutosha ili kuhakikisha ushindi wa Raila, akisema hapaswi kulaumiwa kwa matokeo hayo. Rais William Ruto alitangazwa mshindi baada ya kupata asilimia 50.49 na Raila asilimia 48.85 ya kura.


UHURU KENYATTA – RAILA