Mpango wa kitaifa wa chakula shuleni nchini Kenya unakabiliwa na upungufu wa ufadhili wa Sh bilioni 6 , Mke wa Rais Rachel Ruto amesema. Akizungumza mjini New York, Mke wa Rais alitoa wito wa ushirikiano wa kimataifa ili kuunga mkono upanuzi wa mpango huo, hasa katika kaunti kame na nusu ukame. Alisema chakula shuleni kinaweza kushughulikia njaa huku kikiwaunga mkono wakulima, kujenga ustahimilivu wa jamii na kuboresha matokeo ya kujifunza kwa watoto.