Mke wa Rais Rachel Ruto anasema Kenya inaimarisha hatua za kuwalinda watoto dhidi ya unyanyasaji, dhulma na kuhadaiwai mtandaoni. Akizungumza katika kongamano la Umoja wa Mataifa jijini New York, aliangazia sheria ikiwemo Sheria ya Watoto, Sheria ya Matumizi Mabaya ya Kompyuta na Uhalifu wa Mtandaoni na Sheria ya Ulinzi wa Data. Pia alitaja mpango wa kitaifa unaolenga unyanyasaji wa kingono wa watoto mtandaoni, pamoja na programu za kidijitali za kusoma na kuandika kwa watoto, wazazi na walimu.