Katibu wa wa Elimu ya Juu, Beatrice Inyangala, ameeleza wasiwasi wake kuhusu usalama vyuoni, akibaini kuwa asilimia 90 ya wanafunzi hukumbana na vitendo vya ukatili mtandaoni au wa kimwili, wakiwa wahanga au wahusika. Akizungumza katika hafla ya kufuzu ya Jukwaa la Wasomi, Inyangala alisisitiza kuwa wanafunzi wa kike hubeba mzigo mkubwa zaidi, huku akionyesha hitaji la dharura la kuimarisha usalama katika taasisi hizo na kutumia njia mbadala za kutatua migogoro.
BEATRICE INYANGALA – VIOLENCE