Wanafunzi 8 wa Utumishi Girls wanaotuhumiwa kuwaua wenzao katika mkasa wa moto watabaki kizuizini baada ya Mahakama Kuu kuwanyima dhamana. Jaji Diana Kavedza aliamua kwamba kuachiliwa mara moja kwa washukiwa hao kutawaweka katika hatari kubwa ya madhara. Mahakama ilibaini kuwa kuna haja ya kuwalinda watoto na watu wengine walio katika mazingira magumu, kulinda usalama wa umma, na kuhakikisha uadilifu wa kesi na ustawi wao na ulinzi wa kisaikolojia.

DIANA KAVEDZA – DENY