Mbali na kutoa elimu, vyuo vikuu vina jukumu muhimu katika kuhakikisha kuwa nchi inashinda vita dhidi ya ufisadi. Katibu katika Wizara ya Haki, na Masuala ya Katiba, Judith Pareno, anasema vyuo vikuu vina fursa ya kuimarisha uadilifu kwa kukuza uadilifu wa kitaaluma, kuweka mifumo ya ndani ya kuripoti utovu wa nidhamu, kuingiza masuala ya maadili katika programu za kitaaluma, na kuhimiza ushiriki wa wanafunzi katika masuala ya uongozi, miongoni mwa mambo mengine.

JUDITH PARENO – UNIVERSITIES