Shirika la UNAIDS linasema litatumia Mkutano Mkuu wa 81 wa Umoja wa Mataifa kushinikiza hatua madhubuti zaidi za kimataifa dhidi ya virusi vya HIV na katika maandalizi ya kukabiliana na mikurupuko ya magonjwa. Ajenda hiyo inajumuisha majadiliano kuhusu masuala ya madeni, maendeleo na ukosefu wa usawa, pamoja na uzalishaji wa dawa katika ngazi ya kikanda. Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na mikurupuko ya magonjwa umepangwa kufanyika Ijumaa hii, sambamba na mazungumzo kuhusu kuimarisha mwitikio endelevu wa kimataifa dhidi ya HIV.