Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta anatarajiwa kukabidhi wadhifa wake wa uenyekiti wa muungano wa Azimio la Umoja kwa Gavana wa Siaya, James Orengo, kufuatia mabadiliko katika uongozi wa muungano huo. Vyanzo vinaeleza kuwa Uhuru alimkabidhi Orengo jukumu hilo baada ya mkutano wa viongozi wakuu wa muungano huo uliofanyika jana. Mabadiliko hayo yanakuja baada ya Azimio kubadili jina na kuwa 'Ukombozi Alliance', huku vyama wanachama vikikubaliana kutumia jina hilo jipya na kumteua Uhuru kuwa mwenyekiti wake.