Cole Palmer na Declan Rice ni miongoni mwa wachezaji watano waliojiondoa kwenye kikosi cha Uingereza kutokana na majeraha madogo. Wengine waliojiondoa ni Tino Livramento pamoja na wachezaji wawili wa Manchester United, Kobbie Mainoo na Marcus Rashford, huku Morgan Gibbs-White na James Garner wakijumuishwa kikosini kuchukua nafasi zao. Beki wa kulia wa Real Madrid, Alexander-Arnold, anarejea kikosini baada ya kukosa Kombe la Dunia, huku kinda wa Liverpool, Rio Ngumoha, akiitwa kwa mara ya kwanza. Uingereza itawakaribisha mabingwa wa dunia, Uhispania, katika Nations League uwanjani Wembley Jumamosi kabla ya kuminyana na Czech Jumanne ijayo.
Timu ya vijana ya Kenya, Junior Stars, itafahamu wapinzani wake katika michuano ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ya vijana wa U-17 ya mwaka 2027 (kanda ya CECAFA) kesho, wakati droo itakapofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Droo hiyo itahusisha timu 10: Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Djibouti, Somalia, Sudan na Sudan Kusini. Michuano hiyo ya kufuzu itafanyika Kigali, Rwanda, kuanzia tarehe 10 hadi 20 Oktoba, ambapo timu tatu za juu zitafuzu kwa fainali za AFCON U-17 za mwaka 2027. Junior Stars ilimaliza katika nafasi ya nne kwenye michuano hiyo mwaka uliopita, ikikosa kufuzu kwa AFCON kwa tofauti ndogo sana.
Vipindi vya anga kavu vinahsuhudiwa Kisumu, Eldoret na Kakamega.
Ili kupata habari zadi tembelea tovuti ya radiojambo.