Rais William Ruto ametetea mfumo wa uagizaji mafuta wa serikali kwa serikali, akisema umeiwezesha nchi kupata bidhaa za petroli kwa gharama ya ushindani zaidi kuliko nchi jirani. Akizungumza aliposhuhudia utiaji saini wa Azimio la Pamoja la Nia na Serikali ya Kenya, Umoja wa Mataifa nchini Kenya na Equity Group huko New York, Rais alisema mfumo wa Kenya ulikuwa bora kuliko mfumo unaotumiwa na Uganda kwa sasa, akiwataka wakosoaji kulinganisha gharama ya petroli inayosafirishwa kwa nchi hizo mbili.

WILLIAM RUTO – G-TO-G