Kutokuwa na chama cha kisiasa wala miundo ya mashinani kwa Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna, kunazua maswali kuhusu utayari wake wa kuwania urais. Mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Javas Bigambo, anasema Sifuna anapaswa kuonyesha kasi, rasilimali, na ajenda mbadala ya uongozi na utawala ili kudhihirisha kuwa yuko tayari kwa kinyang'anyiro hicho. Aidha, Bigambo anapinga ulinganifu wowote kati ya Sifuna na Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama, akisema kuwa Obama alikuwa amejenga miundo ya kisiasa ambayo Sifuna bado hajaonyesha kuwa nayo.
JAVAS BIGAMBO- SIFUNA