Kamati mbili za Seneti zinatoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka ili kukamilisha mazishi ya miili 443 ya wahanga wa Shakahola, ambayo bado imehifadhiwa katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Malindi. Maseneta hao wanasema kuwa uchunguzi na vipimo vya DNA umekamilika, na jamaa wa wahanga 14 wameshatambuliwa. Kamati hizo zinataka kuwepo kwa mawasiliano mapana zaidi ili kuwafikia jamaa wa wahanga kabla ya miili iliyosalia kuzikwa, zikisisitiza kuwa mchakato huo lazima ufanyike kwa kuzingatia sheria na heshima.

VOX POP – BODIES