Naibu Rais Kithure Kindiki amewataka viongozi wa eneo la Mlima Kenya kuwaheshimu wazee na kuzingatia wito wao wa umoja. Kindiki alisema wazee wana jukumu la kipekee katika kulinda umoja wa jamii kwa sababu, tofauti na wanasiasa, hawashindani kuwania nyadhifa za kuchaguliwa au kutafuta ushawishi wa kisiasa. Kindiki alisema amekubali jukumu walilompa wazee wa eneo hilo la kuongoza juhudi za maridhiano na umoja, na akaahidi kuheshimu mwongozo wao.

KITHURE KINDIKI – WAZEE