Katibu wa Masuala ya Vijana, Fikirini Jacobs, anasema uchaguzi wa Baraza la Kitaifa la Vijana utawapa vijana wa Kenya fursa ya kushiriki katika uongozi. Jacobs anasema uchaguzi huo—uliopangwa kufanyika Oktoba tarehe 6 katika ngazi ya wadi, Oktoba 19 katika ngazi ya eneo bunge, na Oktoba 30 katika ngazi ya kitaifa—unakuja baada ya kusubiri kwa miaka 14. Anasema mchakato huo utasaidia kuimarisha uwakilishi wa vijana na kusikika zaidi kwa sauti zao katika masuala ya kitaifa.


FIRIKINI JACOBS – ELECTIONS