Wakenya sasa wanaweza kupata huduma za ambulensi bila malipo kwa kupiga simu kwa nambari ya dharura ya 922, chini ya mpango unaotekelezwa na SHA. Mkurugenzi Mtendaji wa SHA Mercy Mwangangi anasema Kituo cha Kitaifa cha Usambazaji wa Ambulensi kinaratibu huduma hiyo, huku SHA ikiwalipa watoa huduma za ambulensi walioidhinishwa. Mwangangi anasema zaidi ya ambulensi 700 kote nchini kwa sasa zimesajiliwa chini ya mpango huo.

MERCY MWANGANGI – AMBULANCES