Tume ya EACC inasema inaimarisha juhudi za kuzuia ufisadi kwa kubaini mianya iliyopo katika taasisi za serikali. Makamu Mwenyekiti wa EACC, Monica Muiru, anasema tume hiyo imefanya ukaguzi na mapitio ya mifumo 41, pamoja na tathmini ya hatari za ufisadi na majaribio ya uadilifu. Muiru anasema EACC inashirikiana na taasisi za serikali, watu binafsi na washirika wengine ili kubaini na kushughulikia hatari za ufisadi kabla ya rasilimali za umma kupotea.
MONICA MUIRU – CORRUPTION