Katibu wa usalama Raymond Omollo, amewahimiza Wakenya kujiandikisha na Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA), akisema kuwa mageuzi ya serikali katika sekta ya afya yanalenga kupunguza mzigo wa gharama za matibabu kwa familia. Akizungumza jijini Narok, Omollo alisema kuwa zaidi ya Wakenya milioni 33 wamesajiliwa na SHA, jambo linalowawezesha kupata huduma za afya bila kujali kama wameajiriwa rasmi au la.
RAYMOND OMOLLO - AFYA