Kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua amewapuuza wazee waliomuidhinisha Naibu Rais Kithure Kindiki kama msemaji wa eneo la Mlima Kenya, akiwaelezea kama wazee bandia. Akizungumza Marekani, Gachagua alidai wazee hao walikusanyika baada ya jaribio linalodaiwa la kugawanya eneo la Mlima Kenya katika kambi mbili, Mlima Kenya Mashariki na Mlima Kenya Magharibi, kushindwa. Alidai baadhi ya wazee walimwambia kwamba waliletwa kwenye mkutano bila kuelewa madhumuni yake na walipewa Sh3,000 ili warudi nyumbani.
RIGATHI GACHAGUA - FAKE