Kundi la viongozi wa dini ya Kiislamu limewataka viongozi wa kisiasa kuchukua hatua za makusudi katika kuhimiza amani huku nchi ikijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027. Wakiongozwa na Abubakar Bini, viongozi hao waliwaonya wanasiasa dhidi ya kutumia wahuni kuvuruga mikutano ya wapinzani wao, wakisema vitendo hivyo vinaweza kuleta madhara makubwa na kuisukuma nchi katika hali ya kuvunja sheria.