Polisi wanachunguza tukio ambapo raia wawili wa Uchina na dereva wao Mkenya wanadaiwa kuporwa shilingi milioni 3.9 baada ya kundi la wanaume waliojifanya kuwa maafisa wa polisi kulizuia gari lao katika barabara ya Nairobi-Keroka, Kaunti ya Nyamira. Polisi walisema tukio hilo liliripotiwa Jumamosi. Kulingana na polisi, waathiriwa walikuwa wakisafiri kupitia eneo la Mekenene walipopitwa na gari aina ya Probox lililowalazimisha kusimama na kisha watu wawili wakashuka na kuanza kuwapora.