Waziri wa Usalama, Kipchumba Murkomen, ametetea azma ya Kenya ya kuandaa Mashindano ya Dunia ya Riadha ya mwaka 2029 kufuatia madai ya matumizi ya dawa za kusisimua misuli  yaliyoibuliwa na baadhi ya wakosoaji. Waziri huyo alipuuzilia mbali madai hayo, akisisitiza kuwa serikali imekuwa wazi katika vita dhidi ya matumizi ya dawa hizo na kuongeza kuwa madai hayo hayana msingi wowote.

KIPCHUMBA MURKOMEN - DOPING