Maseneta wanawake wameonyesha ghadhabu kufuatia ripoti kwamba wanafunzi 36 wa kike kutoka Webuye, Kaunti ya Bungoma, wamepachikwa mimba. Kupitia chama chao, KEWOSA, wabunge hao wametaka kufanyika kwa uchunguzi wa haraka na kukamatwa kwa wahusika wote. Walisisitiza umuhimu wa kuwalinda wasichana dhidi ya unyonyaji na kuhakikisha wanaendelea na masomo, wakisema kuwa elimu inawapa fursa ya kuboresha maisha yao na kujihakikishia maisha ya baadaye yaliyo bora na yenye heshima.