Gavana wa Laikipia, Joshua Irungu, amewataka wagombea wanaotaka kumrithi na wale wanaolenga nyadhifa mbalimbali za kuchaguliwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027 kuendesha kampeni za amani na kuepuka siasa za mgawanyiko. Irungu aliwahimiza wanasiasa kuwa waangalifu na kauli zao, huku akionya dhidi ya kuchochea upya mivutano ya kisiasa iliyoshuhudiwa katika chaguzi zilizopita.
JOSHUA IRUNGU-ASPIRANTS