Watoto wawili wenye umri wa miaka mitatu na mitano walifariki baada ya moto kuzuka nyumbani kwao Ndenderu, kaunti ya Kiambu, Jana alasiri. Kulingana na polisi, moto huo ulitokea yapata saa kumi jioni mnamo katika eneo la Kanisa Katoliki la Ndenderu. Maafisa wa polisi walijibu tukio hilo na kubaini kuwa watoto hao walikuwa ndani ya nyumba hiyo ya mbao na mabati na kukodishwa na mama yao mwenye umri wa miaka 24. Polisi walisema mama huyo alikuwa amewaacha watoto hao peke yao ndani ya nyumba yapata saa moja asubuhi ili kwenda kazini.