Baadhi ya wazee wa Mlima Kenya wamempendekeza Naibu Rais Kithure Kindiki kuwa msemaji na mwakilishi wa eneo hilo katika kuendeleza maslahi na matarajio yake. Wazee hao walitoa tamko hilo jana wakati wa mkutano katika Uwanja wa Kirigiti huko Kiambu, ambapo mashirika kadhaa yanayowakilisha jamii kutoka eneo la Mlima Kenya yalikusanyika. Katika tamko hilo, wazee hao walisema wamejitolea kudumisha umoja miongoni mwa jamii za Agikuyu, Ameru, Aembu na Ambeere.

NELSON MURIU - REAFFIRM