Timu ya soka ya Kenya ya vijana wa U20, jana iliondolewa kwenye mechi za kufuzu kwa CECAFA U20 AFCON baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Sudan Kusini katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Kenya ilimaliza ya pili katika kundi C ikiwa na pointi moja baada ya kufungwa 2-0 na Burundi waliofika nusu fainali siku ya Alhamisi. Uganda itamenyana na Sudan katika nusu fainali, huku wenyeji Tanzania wakicheza dhidi ya Burundi katika nusu fainali ya pili. Timu zilizofika fainali zitafuzu moja kwa moja kwa Kombe la Mataifa ya Afrika la 2027.

Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi, Narok na Kajiado.

Ili kupata habari zaidi tembeleatovuti ya radiojambo.