Mwanzo wa ushindi wa Arsenal msimu huu ulifika kikomo kufuatia kichapo cha 3-0 kutoka kwa Brighton kwenye Uwanja wa Amex jana. Pascal Gross na Kostoulas waliiweka Seagulls mbele 2-0 kufikia muda wa mapumziko, kabla ya Andres Baixauli kuongeza la tatu dakika ya 57. Matokeo hayo yaliifanya Brighton kupanda hadi nafasi ya nne kwenye jedwali wakiwa na pointi 10 huku wakisherehekea kumbukumbu yao ya miaka 125, huku Arsenal ikishuka hadi nafasi ya pili.
Wakati huo huo, Everton iliwashinda Ipswich wenye wachezaji 10 1-0 huku Newcastle ikiwashinda Hull City 2-1 nayo Aston Villa ikiifunga Tottenham 3-2. Mechi nyingine ya siku ya tano iliwashuhudia Coventry wakiishinda Nottingham 1-0 na kuwa ushindi wao wa kwanza msimu huu na kusonga nafasi mbili kutoka chini.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Kitale, Kisii na Kericho.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.