Naibu Rais Kithure Kindiki amesema amewasamehe wapinzani wa kisiasa ambao wamemtukana, akiapa kutii ushauri wa wazee na kuepuka migongano ya kisiasa. Kindiki alisema hatajibu tena matusi kutoka kwa wapinzani wa kisiasa, akiwahimiza viongozi kuuza sera zao badala ya kushambuliana. Alisema ametukanwa mara kadhaa na watu aliowaheshimu na kufanya nao kazi lakini amechagua kupuuza mashambulizi hayo.
KITHURE KINDIKI - KETI