Mgombea wa kiti cha ugavana wa Mombasa, Suleiman Shahbal, ameahidi kuanzisha vituo vya huduma jumuishi kwa jamii katika wadi zote 30 ili kuinua viwango vya elimu, kukuza vipaji na kuwaepusha vijana na matumizi ya dawa za kulevya. Akizungumza katika mkutano wa mashauriano na viongozi wa dini ya Kikristo, alibaini kuwa viwango vya wanafunzi wanaohama kutoka shule za umma kwenda vyuo vikuu bado ni vya chini ikilinganishwa na shule za binafsi. Mbunge huyo wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) alisema vituo hivyo pia vitawaandaa watahiniwa kwa ajili ya mitihani ya kitaifa na kuboresha nafasi zao za kuendelea na elimu ya juu.
Advertisement
September 20, 2026
1 min read
Related Topics
Facebook
Loading...
Loading next article...
You've reached the end
Browse all articles
Advertisement
Suggested Articles
Newsletter
Get the latest sports stories delivered straight to your inbox.
Now Playing