Serikali inaimarisha uwezo wa sekta ya kilimo cha bustani kuhimili mabadiliko ya haliya anga na misukosuko katika masoko ya kimataifa. Akizungumza katika maonyesho ya sekta ya kilimo cha bustani mjini Naivasha, Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe alisisitiza umuhimu wa kufanya utafiti kuhusu aina za mazao zinazoweza kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa na teknolojia mpya ili kulinda uzalishaji wa siku zijazo. Pia alitangaza mipango ya kuanzisha kitengo cha kuratibu uhusiano na sekta binafsi ndani ya shirika la KALRO ili kuimarisha ushirikiano kati ya watafiti na wadau wa sekta hiyo.
MUTAHI KAGWE - DECISION