Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen amelaani vikali ongezeko la visa vya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na wazee katika Kaunti ya Nyeri. Akizungumza katika kaunti hiyo, Murkomen aliwaonya wakaazi dhidi ya kutatua unyanyasaji wa kijinsia nyumbani, akisisitiza kwamba kila mshukiwa lazima apelekwe mahakamani. Alisisitiza kwamba jamii lazima ifanye kazi pamoja ili kuweka familia na wazee salama na kuheshimiwa.

KIPCHUMBA MURKOMEN - GBV