Mbunge wa Khwisero, Christopher Aseka, ametoa wito kwa familia zinazoishi kando ya Mto Yala na maeneo mengine yanayokumbwa na mafuriko kuhamia maeneo ya juu kabla ya mvua inayotarajiwa ya El Niño kunyesha. Aliwasihi wakaazi kuchukua hatua mapema ili kulinda maisha na mali huku mvua ikizidi. Aseka alisema Serikali inashirikiana na mashirika ya kibinadamu ili kuimarisha utayari wa majanga na kuhakikisha jamii zilizo hatarini zinapata msaada kwa wakati unaofaa.
CHRISTOPHER ASEKA - MVUA