Mbunge wa Ndia George Kariuki na Mbunge wa Juja George Koimburi wamepinga kuidhinishwa kwa Naibu Rais Kithure Kindiki kama msemaji wa Mt Kenya, wakisema viongozi na wakaazi wa eneo hilo hawakushauriwa. Kariuki alikosoa mkutano huko Kirigiti ambapo Kindiki aliwasilishwa kama kiongozi wa eneo hilo, akisema ni viongozi wachache sana waliochaguliwa walioshiriki. Koimburi alimshutumu Kindiki kwa kufanya mikutano katika maeneo bunge yao bila kwanza kushauriana na viongozi waliochaguliwa wanaowawakilisha.

KOIMBURI KARIUKI - ENDORSEMENT