Ni kinyume cha imani ya Kiislamu kwa viongozi wa kidini kuwashauri waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia kuendelea katika ndoa au mahusiano ya unyanyasaji. Katibu Mkuu wa CIPK Mohamed Halifa anasema ushauri kama huo unakuza unyanyasaji, akibaini kuwa wanawake Waislamu wana haki ya kutafuta talaka katika hali kama hizo. Anasema viongozi wa kidini wanaendelea kuwashauri waumini dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia ili kusaidia kujenga familia salama na zenye nguvu.

MOHAMED HALIFA - VICTIMS