Mahakama Kuu mjini Murang'a imesimamisha Ligi Kuu ya Kenya kuanza leo kama ilivyopangwa. Jaji Dorah Chepkwony ameamua kwamba msimu wa mwaka 2026/27 hauwezi kuanza bila mechi ya mchujo kati ya Kariobangi Sharks na Mombasa United. Amri hiyo inafuatia ombi la Evans Nduta kupinga kuanza kwa msimu, pamoja na kesi yake ya msingi ya kupinga matumizi ya Sheria za FKF za 2025.
Bado haijabainika kama FKF itafuata amri ya hivi karibuni ya mahakama. Wakati wa mkutano na wenyeviti wa matawi mapema wiki hii, Rais wa FKF Hussein Mohammed alionyesha kwamba hataheshimu amri za mahakama za kusimamisha shughuli za soka kuendelea.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Kitale, Kisii na Kakamega.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambp.