Timu za netiboli za wanawake na wanaume za Kenya zinaanza michuano yao ya Netiboli ya Afrika katika uwanja wa ndani wa Kasarani. Timu ya wanawake itaanza kampeni yao dhidi ya Nigeria kabla ya kukabiliana na Uganda, Malawi na Zambia katika kundi A. Wakati huo huo, timu ya wanaume itakuwa ikifungua kampeni yao dhidi ya Uganda huku Afrika Kusini, Eswatini, na Malawi zikisubiri katika kundi B. Nahodha wa timu ya wanawake Parin Simiyu anasema wako tayari na amewasihi mashabiki kujitokeza kwa wingi na kuwaunga mkono.

Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Makindu, Voi na Mariakani.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.