Rais William Ruto anasema serikali imewekeza Sh bilioni 21 kati ya Sh30 bilioni zilizotengwa kwa Programu ya Uboreshaji wa Polisi. Ruto alisema programu hiyo inawapa maafisa wa polisi vifaa vya kisasa, teknolojia na uwezo wa kuboresha utoaji wa huduma. Akizungumza katika Chuo cha Kitaifa cha Polisi huko Utawala, alisema serikali pia inajenga nyumba 28,000 nchini kote ili kuwapa maafisa na familia zao makaazi mazuri.
WILLIAM RUTO - MODERNIZATION