Polisi na maafisa wa utawala wameanzisha uchunguzi baada ya wasichana 36 katika shule moja huko Webuye, Kaunti ya Bungoma, kupata mimba, huku mamlaka zikitafuta kuwatambua waliohusika. Mkuu wa shule alisema wasichana 13 tayari wamejifungua, 13 wana ujauzito, huku 10 wakiacha shule baada ya kupata mimba. Kamishna Msaidizi wa Kaunti ya Webuye Mashariki, Emmanuel Kenga, alisema polisi wanafanya uchunguzi ili kubaini kilichotokea na kuwakamata watakaopatikana na hatia.
EMMANUEL KENGA - MIMBA