Mkurupuko wa Ebola nchini D.R Congo haujaisha bali unaenea katika sehemu mpya za nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati, Doctors Without Borders imeonya. Naibu mkurugenzi wa shughuli wa MSF Guyguy Manangama anabaini kuwa sehemu kubwa ya janga la hivi karibuni, limejikita katika maeneo magumu kufikiwa kaskazini na mashariki ambayo kwa muda mrefu yamekumbwa na ukosefu wa utulivu na vikundi vyenye silaha. Tangu kutangazwa katikati ya Mei, virusi hivyo hatari vimewaua zaidi ya watu 3,600 kati ya maambukizi 7,200 yaliyorekodiwa.