Naibu Rais Kithure Kindiki amewapa changamoto viongozi wa kisiasa wanaotafuta nafasi za kuchaguliwa kufanya kampeni kwa rekodi yao ya maendeleo badala ya kutukanana. Akizungumza baada ya kukagua miradi ya maendeleo huko Mwea, Kaunti ya Kirinyaga, Kindiki alisema ushindani wa kisiasa unapaswa kuwapa viongozi nafasi ya kuelezea kile walichowafanyia watu, akibaini kuwa Wakenya hatimaye watatumia haki yao ya kidemokrasia kuchagua viongozi wanaowataka.
KITHURE KINDIKI - MATUSI