Madereva wanaotumia Barabara Kuu ya Nairobi kutoka James Gichuru kuelekea katikati mwa jiji wanahimizwa kutumia barabara ya chini kwenye Waiyaki Way kutokana na matengenezo ya muda na ujenzi kwenye sehemu ya juu ya daraja la juu kwenye lango la Westlands. Kulingana na taarifa ya umma iliyotolewa na kampuni ya expressway, kazi hizo zitaanza leo jioni hadi Jumatatu mchana. Madereva wameshauriwa kuwa waangalifu na kufuata maagizo kutoka kwa maafisa wa trafiki kwenye njia hiyo.