Wakaazi wa wadi ya Karumandi katika Kaunti ya Kirinyaga hawatalazimika tena kusafiri umbali mrefu kupata huduma za matibabu kufuatia kufunguliwa kwa zahanati mpya inayotarajiwa kuhudumia takriban watu 5,000. Zahanati ya Kavote, iliyozinduliwa rasmi na Gavana Anne Waiguru, itatoa huduma kwa wagonjwa, huduma za afya ya mama na mtoto, maabara, dawa, pamoja na huduma za kinga dhidi ya magonjwa. Kituo hicho kinatarajiwa kupunguza mzigo kwa wakaazi ambao hapo awali walilazimika kusafiri zaidi ya kilomita tano ili kupata huduma za msingi za afya.


ANNE WAIGURU - HOSPITAL