Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja amewasihi wamiliki wa mali kulipa ada za ardhi ili kuiwezesha kaunti kufadhili huduma muhimu na miradi ya maendeleo. Sakaja anasema ni wamiliki elfu 50 pekee kati ya wamiliki elfu 250 waliosajiliwa wanaolipa ada kwa sasa. Alisema ada zisizo lipwa zinakwamisha huduma kama vile ukusanyaji wa taka, huduma za afya na ukarabati wa barabara.
JOHNSON SAKAJA - TASTE