Kipa Luca Zidane hakujumuishwa katika kikosi cha Algeria kwa ajili ya mechi za kufuzu AFCON ya mwaka 2027 dhidi ya Zambia na Burundi. Luca, ambaye ni mwana wa gwiji wa soka la Ufaransa, Zinedine Zidane, anatumikia adhabu ya kutocheza mechi mbili kufuatia tukio la ugomvi lililotokea katika michuano iliyopita ya AFCON. Hata hivyo, kikosi cha Algeria bado kimejaa wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu. Rayan Ait Nouri wa Manchester City anaongoza kikosi hicho cha wachezaji 27, akiwa pamoja na Rami Bensebaini, Amine Gouri, na Mohamed Amin, miongoni mwa wengine.
Nahodha wa Misri, Mohamed Salah, amejumuishwa katika kikosi cha 'The Pharaohs' kwa ajili ya raundi ya kwanza na ya pili ya michuano ya kufuzu AFCON ya mwaka 2027, ambapo Misri itakabiliana na Angola pamoja na Sudan Kusini. Salah anaongoza safu ya washambuliaji, akiwa sambamba na Omar Marmoush, Mostafa Zico, na Abdel Karim, huku 'The Pharaohs' wakianza maandalizi ya kampeni yao ya kufuzu. Mara ya mwisho kwa 'The Pharaohs' kutwaa taji la AFCON ilikuwa mwaka 2010, na sasa wanalenga kufuzu kushiriki michuano hiyo itakayofanyika Afrika Mashariki.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi, Narok na Kajiado.
Ili kpata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.