Timu ya taifa ya voliboli ya wanaume ilipata kichapo chake cha pili mfululizo katika Mashindano ya Voliboli ya Mataifa ya Afrika jijini Tunis, baada ya kufungwa na Ghana jana. Wafalme Stars walipoteza kwa seti za 25-20, 25-23, na 25-20, na hivyo kupata kichapo kingine cha seti 3-0 kufuatia kufungwa Jumatano na wenyeji Tunisia. Matokeo hayo yaliwaacha Wafalme mkiani mwa Kundi A lenye timu tatu, wakiwa hawana hata pointi moja. Kenya, ambayo ilishika nafasi ya tisa katika mashindano mawili yaliyopita, itachuana na Algeria Jumapili katika hatua ya 16 bora.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Mombasa, Kilifi na Malindi.
Ili kupata habari zadi tembelea tovuti ya radiojambo.