Baada ya ligi ya KPL kuahirishwa mara mbili kutokana na migogoro na kesi mahakamani, hatimaye ligi hiyo inaanza kesho, huku Gor Mahia wakianza kampeni yao ya kutetea ubingwa dhidi ya Muranga Seal katika Uwanja wa Nyayo. Ulinzi Stars watawakaribisha Tusker, huku Mathare United wakiminyana na APS Bomet na Posta Rangers wakichuana na Shabana. Siku ya Jumapili, wageni ya 3K FC watakabiliana na Mara Sugar, Nairobi United wakicheza dhidi ya KCB, na Migori Youth wakivaana na Kenya Police. AFC Leopards watahitimisha mechi za raundi ya kwanza kwa kucheza dhidi ya Bandari katika Uwanja wa Nyayo.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Makindu, Voi na Mariakani.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.