Kocha Mkuu wa timu ya Rising Stars, Gilbert Selebwa, anasema kuwa licha ya kufungwa mabao 2-0 na Burundi katika mashindano ya CECAFA U20 jijini Dar es Salaam jana, vijana wake walicheza vizuri lakini hawakuwa na bahati dhidi ya wapinzani wao. Selebwa anaamini kuwa amebaini udhaifu wa timu yake katika mechi hiyo ya kwanza ya mashindano na atafanyia marekebisho makosa hayo kabla ya kuwakabili Sudan Kusini kesho katika mechi ya mwisho ya Kundi C, ambapo ushindi utawapa nafasi ya kufuzu kwa hatua ya nusu fainali. Timu zitakazofika fainali zitafuzu kwa michuano ya AFCON ya mwaka 2027.
GILBERT SELEBWA - CECAFA
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Machakos, Kibwezi na Kitui.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.