Naibu Rais Kithure Kindiki ameapa kuwapuuza wakosoaji wanaotaka kumkengeusha asiwaletee maendeleo watu wa Kenya. Kindiki amesema analenga kikamilifu kumsaidia Rais William Ruto kukamilisha miradi ya maendeleo na kuzindua zaidi katika kila sehemu ya nchi kwa lengo la kuboresha maisha ya Wakenya wote. Akizungumza huko Maua, Kaunti ya Meru, Kindiki pia alisema amewasamehe viongozi kutoka kaunti hiyo ambao wamekuwa na tabia ya kumtukana.
KITHURE KINDIKI - KELELE