Mwakilishi wa Wanawake wa Uasin Gishu, Gladys Shollei, anataka vitengo vya polisi vinavyoshughulikia masuala ya kijinsia vihamishiwe katika vituo vya afya ili kurahisisha waathiriwa wa ukatili wa kijinsia kuripoti visa hivyo. Shollei, alisema waathiriwa hawapaswi kulazimishwa kuripoti visa hivyo katika vituo vya polisi. Pia alitoa wito wa kuwepo kwa vituo salama vya kuhifadhi waathiriwa wa ukatili wa kijinsia katika kila kaunti.
GLADYS SHOLLEI - REPORTING