Waziri wa Elimu Julius Ogamba amewahakikishia wanafunzi kuwa serikali inafanya mapitio ya mfumo wa ufadhili wa elimu ya juu ili kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayekosa fursa kutokana na changamoto za kifedha. Akizungumza katika hafla ya kufuzu ya Chuo Kikuu cha Nairobi, Ogamba alisema kuwa Mswada uliopendekezwa ambao kwa sasa unashirikisha maoni ya umma — unalenga kutoa ufadhili kamili kwa wanafunzi waliopewa nafasi katika vyuo vikuu, KMTC, TVET na TTC.
JULIUS OGAMBA - FINANCING